Huheso FM

Maafisa wa majeshi wafanya usafi, kutoa msaada hospitali ya Kahama

September 13, 2024, 3:54 pm

Jeshi la polisi wakikabidhi vitu mbalimbali kwa Hosiptali ya Wilaya Kahama

Jeshi la polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kwa pamoja wamefanya usafi wa mazingira na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.

Na Paschal Malulu-Huheso FM

Zoezi hilo limefanyika Septemba 13, 2024 lengo likiwa ni kuadhimisha siku ya Jeshi la Polisi kutimiza miaka 60 baada ya ukoloni.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo chupa za kuchemshia maziwa ya watoto njiti, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Mtaju Mwayombo amesema wameguswa kushiriki siku ya polisi kwa kushiriki na jamii.

Sauti ya Mkuu wa kituo cha polisi Kahama, Mtaju Mwayombo

Akitoa shukrani zake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Daniel Mzee amepongeza jitihada hizo kuwa wamekuwa wakishirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama katika shughuli mbalimbali hivyo ameiomba jamii kuunga nguvu hiyo.

Sauti ya Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Dkt. Daniel Mzee akitoa shukrani zake kwa jeshi la polisi

Pia Jeshi la polisi limetoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva wanaosafirisha abiria kutoka mjini Kahama kwenda maeneo mbalimbali katika kituo cha mabasi CDT kuzingatia sheria za usalama barabarani Pamoja na kuvaa sare.

Hata hivyo vyombo hivyo vya ulinzi na usalama Jeshi la Polisi, Magereza na Zimamoto na uokoaji kwa Pamoja vimeiomba jamii kujiepusha na uvunjifu wa amani sambamba na kufichua vitendo vya uhalifu.