Huheso FM
Huheso FM
June 14, 2025, 10:09 am

Sherehe za miaka 43 ya Sungusungu mjini Shinyanga zimefanyika mjini Shinyanga kwenye Kata ya Iselamagazi huku wakiaswa kulinda amani ya nchi
Na Neema Nkumbi
Jeshi la Jadi la Sungusungu Wilaya ya Shinyanga Vijijini Juni 12, 2025 limeadhimisha miaka 43 tangu kuanzishwa kwake kwa sherehe iliyoambatana na ujumbe wa kuendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha ulinzi wa watu na mali unaimarika zaidi katika vijiji.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga mgeni rasmi, Afisa Mtendaji wa Kata ya Iselamagazi Amos Chacha, amepongeza jeshi hilo la jadi kwa kuendelea kuwa chombo muhimu katika suala la ulinzi wa raia na mali, na kuwasisitiza wanajeshi hao wa jadi kuendelea kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za nchi.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kata ya Iselamagazi yakihudhuriwa na sungusungu kutoka tarafa tatu za Iselemagazi Mashariki, Nhindo Magharibi na Itwangi, wakiongozwa na viongozi wao wa ngazi mbalimbali.