Wananchi wapongeza ulinzi shirikishi kutekeleza majukumu yake
July 30, 2024, 3:04 pm
Wakazi wa Kata ya Nyihogo iliyopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wameonyesha kufurahishwa na utendaji kazi wa Ulinzi shirikishi ambapo kwa asilimia kubwa umeweza kukabiliana na wimbi la vibaka na kuimalisha ulinzi na usalama.
Wakizungumza hii leo wameeleza kuwa ,Ulinzi uliopo umesaidia kwani Vibaka wamepunguza kasi ya matukio ya ajabu na mpaka sasa raia wana amani hata wanapotembea usiku .
Pia wameongeza kuwa Serikali za mitaa zizingatie umri inapopanga vikosi vya ulinzi na kutoa mafunzo kwa Walinzi hao ili kuepuka migogoro inayotokea na Wananchi
Kwa upande wao Wajumbe wamesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha kata hiyo ya Nyihogo inaondokana na Matukio ya kiharifu yakiwemo ya upolaji,ukabaji na ubakaji,na wamesisitiza vijana wafanye kazi halali .
Mwenyekiti Idd Mitimingi ameongeza kwa Kusema kwamba atahakikisha vikosi vya ulinzi vinafanya kazi inavyositahili kwa kuzingatia maadili ya kazi yao na amewaomba Wananchi kutunza mali zao vizuri.