Huheso FM

Muuza Chips mbaroni kwa tuhuma mauaji

May 30, 2024, 12:10 pm

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi

“Tunamshikilia huyu bwana kwa sababu tunafanya uchunguzi na walikuwa na kesi kuhusu hatima ya talaka yao ambayo ilitakiwa itolewe tarehe 28 mwezi huu wa tano hivyo tukikamilisha uchunguzi tutamfikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria”

Na Neema Nkumbi-Huheso FM

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linamshikilia  Jafari Magesa Miaka 31 Mkazi wa Milambo kwa tuhuma za kuunda njama za kumuua mtalaka wake na kitu chenye ncha kali aitwaye Gaudensia Shukuru miaka 25 Mkazi wa Malunga  Manispaa ya Kahama.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea Mei 27, 2024 baada ya kupokea taarifa toka kwa Mwenyekiti wa kitongoji cha Wendele katika Kata ya Wendele Manispaa ya Kahama uwepo wa mwili wa mwanamke aliyeuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali.

SACP Magomi amesema kuwa katika upelelezi wa awali wa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa Talaka kati ya marehemu na aliyekuwa mumewe ambapo walikuwa na kesi Mahakamani juu ya Talaka ambayo ilikuwa itolewe hukumu yake Mei 28, 2024.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi akizungumzia tukio hilo la mauaji