Huheso FM

Watoto wafariki wakiogelea bwawani Shinyanga

May 16, 2024, 6:27 pm

Wananchi na askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji wakitafuta miili ya waototo waliozama kwenye Bwawa la maji Tinde.

Watoto watatu wakazi wa Kata ya Tinde Wilaya ya Shinyanga, Mkoa wa Shinyanga wamefariki dunia baada ya kuzama katika bwawa la Ngaka lililopo katika kijiji cha Nyambuhi walipoenda kuogelea.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio wamesema tukio hilo limetokea Mei 16, 2024 saa nne asubuhi ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kupata mwili wa mtoto mmoja na juhudi za kutafuta miili mingine ya watoto zinaendelea.