Wananchi wasiogope Jeshi la Polisi-RPC Magomi
September 15, 2023, 1:10 pm
Kamanda Janeth Magomi amezungumzia elimu ambayo wamekuwa wakiitoa katika jamii ili kupunguza au kutokomeza matukio ya wizi, uvunjaji na uhalifu vinakwisha ambapo amesema polisi Kata wapo kwenye kila Kata ili kuzngumza na wananchi ili kuwafichua wahalifu na wamekuwa wakitoa elimu hadi mashuleni.
Na, Paschal Malulu-Kahama
Imeelezwa kuwa mtaa wa Nyasubi, kata ya Nyasubi katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga hali ya ulinzi na usalama imekuwa shwari tofauti na hapo awali ambapo matukio ya kihalifu yalikuwa yakijitokeza.
Akizungumzia hali ya usalama wa Mtaa, mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo, Leonard Mayala amesema baada ya kuimarisha ulinzi baadhi ya matukio yamepungua kama vile wizi.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa mtaa wa Nyasubi wameipongeza serikali ya Mtaa kwa kuweka ulinzi na kupelekea kupungua kwa matukio ya uvunjaji yaliyokuwa yakijitokeza kwa baadhi ya watu kuibiwa.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema matukio ya uvunjaji na wizi yamepungua lakini wameendelea kushirikiana na wananchi namna ya kuthibiti matukio hayo.
Aidha serikali ya Mtaa wa Nyasubi imewaomba wakazi wa Mtaa huo kwa ujumla kushiriki katika vikao vya dharura hasa vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuleta amani kubwa kwenye Mtaa.