Bandari tatu zatengewa Bilioni 60
August 31, 2023, 2:24 pm
Waandishi wa Habari mkoani shinyanga wametakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye jamii katika kuizungumzia Bandari na matumizi yake ili wananchi waweze kufahamu matumizi yake na umhimu wake.
Hayo yamesemwa na Afisa Bandari ya Isaka-Kahama mkoani Shinyanga, Abeli Mshang’a wakati akizunguzma na waandishi wa Habari wa Mkoa huo na kubainisha kuwa Bandari hiyo kavu imekuwa ikirahisisha utendaji wa bandari na inahudumia Nchi tano kusafirisha mizigo ikiwemo Rwanda,Burundi,Uganda,Sudani kusini,Na DRC.
Kwa upande wake Meneja wa Bandari Ziwa Victoria Frednand Nyath amesema katika maboresho ya Bandari tatu za Mwanza kaskazini, Kemondo na Bukoba serikali imetenga Bilioni 60 kwa ajili ya kukarabati na maboresho hayo yataongeza ufanisi wa utendaji kazi bandarini.
Aidha miongoni mwa maboresho yanayotarajiwa kufanywa ni Pamoja na gati ya meli ya mizigo ya Gurudumu na majengo ya abiria na kudhibiti mmomonyoko wa udongo kwa kuweka sakafu eneo hilo.