Wajumbe MTAKUWWA wapanga mikakati kupinga ukatili wa kijinsia
July 3, 2023, 12:24 pm
Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekutana katika kikao cha mradi wa Mwanamke Amka ili kujadili mpango kazi ambao utatokomeza ukatili wa kijinsia huku wanaume wakitajwa kuwa ndio chanzo kikubwa kinachochochea ukatili.
Na Misoji Masumbuko
Akizungumza wakati wa kikako kilichofanyika Ghama Hotel mratibu wa mradi wa Mwanamke Amka Joyce Michael amesema wanaume wanatakiwa kuwa wawazi na wakweli katika kuibua vitendo vya ukatili ambavyo vinafanyika kwenye jamii.
wanaume wanatakiwa kuwa wawazi na wakweli katika kuibua vitendo vya ukatili ambavyo vinafanyika kwenye jamii
Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA kutoka kata tofautitofauti wamesema wataendelea kutoa elimu kwenye jamii na kuwafikishia ujumbe ili waondokane na vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto.
Kikao hicho kimejumuisha wanaume ambao ni wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA na madereva bodaboda pamoja na maafisa maendeleo na watendaji kutoka katika kata za Mondo, Zongomela, Kinaga, Ngogwa na Kilago zilizopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.