Wanafunzi na walimu wa clubs za GBV wapanga mpango endelevu wa ulinzi na usalama wa mtoto
March 24, 2022, 6:00 pm
Kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi na usalama wa mtoto ndani na nje ya shule wanafunzi wa clubs za kupinga ukatili wa kijinsia GBV wilayani kahama mkoani shinyanga wamesema imekua chanzo kikubwa kinachosababisha kutendendeka kwa vitendo vya ukatili kwenye jamii.
Wameyasema hayo wakati wa kikao cha Mwanamke Amka kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ghama Hoteli lengo ikiwa ni kutengeneza mpango kazi endelevu wa kulinda ulinzi na usalama wa mtoto.
Wamesema haki za watoto mashuleni zimekua hazitekelezwi kwa kukosa miundo mbinu rafiki za mabweni na uzio ambavyo vitamlinda hivyo kupelekea mimba za utotoni.
Kwa upande wao walimu walezi wa clubs za kupinga ukatili wa kijinsia GBV wamesema watashirikiana na serikali na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha wanalinda usalama wa mtoto ndani na nje ya shule.
Hata hivyo kikao hicho cha Mradi wa mwanamke Amka unaolenga kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na kuratibiwa na Joyce Michael umehusisha wanafunzi na walimu kutoka shule za kata ya Zongomela, Kinaga,Mondo, Ngogwa na Kilago