Wajumbe MTAKUWA wapanga mikakati ya kupinga ukatili wa kijinsia.
March 14, 2022, 1:51 pm
Wajumbe wa kamati ya MTAKUWA Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamekutana katika kikao cha Mradi wa Mwanamke Amka ili kujadili mpango kazi ambao utatokomeza ukatili wa kijinsia huku wanaume wakitajwa kuwa ndio chanzo kikubwa kinacho chochea ukatili.
Akizungumza wakati wa kikako kilichofanyika ghama hoel mratibu wa Mradi wa Mwanamke Amka Joyce Michael amesema wanaume wanatakiwa kuwa wawazi na wakweli katika kuibua vitendo vya ukatili ambavyo vinafanyika kwenye jamii.
Kwa upande wao wajumbe wa Kamati ya Mtakuwa kutoka katika kata tofautitofauti wamesema wataendelea kutoa elimu kwenye jamii na kuwafikishia ujumbe ili waondokane na vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto.
Hata hivyo kikao hicho kimejumuisha wanaume ambao ni wajumbe wa kamati ya Mtakuwa na madereva bodaboda pamoja na Maafisa maendeleo na watendaji kutoka katika kata za Mondo, Zongomela,Kinaga,ngogwa na kilago zilizopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.