Elimu yaendelea kutolewa kupinga ukatili wa kijinsia.
March 12, 2022, 12:09 pm
Ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika manispaa ya kahama Mkoani shinyanga wajumbe wa mradi wa mwanamke amka wametakiwa kuendelea kutoa elimu kwenye jamii hasa kwa watoto walioko mashuleni.
Hayo yamesemwa na mkuu wa dawati la jinsia na watoto polisi Kahama Tiho Masatu katika kikao cha Mradi wa Mwanamke Amka kinacholenga kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kilichofanyika kwenye ukumbi wa ghama hotel.
Tiho amesema elimu ya ukatili ikitolewa kwa wanafunzi katika jamiii itawasaidia kutambua mambo ya ukatili wanayotakiwa kuyaepuka na namna ambavyo wataweza kujilinda kwa jinsia zote za kike na kiume.
Kwa upande wao wajumbe wa mradi wa mwanamke amka wamesema vitendo vya ukatili wa kijinsia vimepungua hivyo wataendelea kutoa elimu kwenye jamii kupitia mafunzo wanayoyapata kwenye mradi huo
Mradi wa Mwanamke Amka unaolenga kupinga ukati wa kijinsia kwa wananawake na watoto unafadhiliwa na The Fondation for Civil Society (FCS) na unatekelezwa shirika la Huheso Foundation katika Kata tano za Zongomela, Kinaga,Ngogwa, Mondo, na Kilago zilizopo Manisapaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.