Huheso FM

Elimu ya hedhi salama kwa wasichana yazidi kutolewa wazazi waungana

May 27, 2021, 8:05 pm

Katika kuelekea siku ya hedhi salama duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi Mei 28 baadhi ya wazazi na walezi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameeleza namna wanavyotoa elimu juu ya makuzi kwa watoto wao wa kike.

Wakizungumza na Huheso fm mapema hii leo wazazi na walezi wamesema wamekuwa wakiwapatia watoto wao mafunzo kuhusu makuzi namna wanapokua hedhi na pale ambapo wanakuwa hawajafikia umri huo pia hupewa mafunzo hayo.

Kwa upande wake Muuguzi kitengo cha vijana upande makuzi katika manispaa ya Kahama, Sibrina Kimaro amesema wazazi na walezi wamekua wakiwapatia elimu kuhusu hedhi salama kwa wasichana ili wanapokua majumbani kwao wawapatie watoto wa kike.

 Maadhimisho ya siku Hedhi duniani mwaka huu yanakaulimbiu isemayo “NIWAKATI WA KUCHUKUA HATUA ILI KUHAKIKISHA VIFAA VYA KUJISTIRI/TAULO ZA HEDHI ZINAPATIKANA KWA URAHISI NA BEI NAFUU KWA MSICHANA/MWANAMKE”.

Hata hivyo waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma mei 24 amesema kuwa tafiti zinaonesha kila siku wanawake zaidi ya million 12 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 wakua kwenye hedhi duniani.