Wilaya ya Kahama inakabiliwa na uhaba wa damu salama
May 13, 2021, 1:01 pm
Hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga inakabiliwa na uhaba wa damu salama huku wananchi wilayani humo wakiombwa kuendelea kujitokeza kuchangia damu.
Hayo yamesema na mratibu wa damu salama hospitali ya Wilaya ya Kahama, God Abdallah amesema uhitaji wa damu ni mkubwa hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kuchangia kwa hiari huku akisema mtu kabla ya kutoa damu vipimo hufanyika ikiwemo wingi wa damu.
Kwa upande wao wakazi wa Manispaa ya Kahama wamesema kuwa suala la uchangiaji wa damu salama sio la serikali ni watu wote ili kusaidia upatikanaji wa damu salama unakuwa rahisi na kuokoa maisha ya watu.
Hata hivyo serikali imekuwa ikitoa elimu mbalimbali namna ya uchangiaji wa damu salama kwa hiari katika maeneo yote.