Huheso FM
Wazee Wilayani Kahama watakiwa kujiwekea akiba ya pesa
May 7, 2021, 1:50 pm
Wazee wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kujiwekea akiba ya pesa ili bima inapoisha muda wake waweze kujilipia wao wenyewe pasipo kusubiri kila mwaka kulipiwa na wadau mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kahama, Yahaya Bundala na kuwataka vijana kuendelea kuwachangia wazee pesa ya bima ya CHF wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea.
Amesema madiwani wawahamasishe wadau mbalimbali katika Kata zao ili waendelee kuwashika mkono wazee ambao hawajapata bima katika maeneo yao.
Hata hivyo mwaka 2018-2021 Manispaa ya Kahama ilifanikiwa kutoa jumla ya shilingi millioni 27 na laki saba kuwapatia CHF kwa ajili ya kuwakatia bima wazee wenye umri kuanzia miaka 60 nakuendelea.