Huheso FM

Utamaduni wa ukeketaji wahatarisha maisha ya watoto wa kike Tarime.

April 12, 2021, 6:38 pm

May be an image of one or more people, people standing, people sitting and outdoors

Kituoa Cha ATFGM Masanga kilichopo wilayani Tarime Mkoani Mara kinasomesha zaidi ya watoto 100 katika shule mbalimbali waliokimbia kufanyiwa ukeketaji.

Meneja Miradi wa ATFGM Masanga, Valerian Mgani amesema miongoni mwa watoto wanaowasomesha familia zao zimekataa kuwapokea kwa kukimbia kufanyiwa ukeketaji kwani jamii hiyo kuwa mtoto wa kike asipofanyiwa ukeketaji husababisha mkosi katika familia.

Mgani amesema msichana anapofanyiwa ukeketaji humsababishia madhara ikiwemo magonjwa ya kuambukizwa kama ukimwi kutokana na zana zinazotumika kutokuwa salama na ni kitendo kisicho cha kitaalam.

 INSERT MGANI-ATFGM………………………………

Kwa upande wake mwanasheria wa kituo hicho Dorah Luhimbo amesema desturi ya ukeketaji wilayani humo bado inaendelea kutokea kutokana kundi la wazee wanaojulikana kama “Ngariba” kuendeleza utamaduni huo ambapo kuna baadhi ya kesi bado zinaendelea mahakamani zinawahusu wazee hao.

INSERT MWANASHERIA……………………………

Kufuatia hali hiyo shirika la TADIO Na C-SEMA Tanzania chini ya ufadhili wa shirika la idadi ya watu duniani  UNFPA limewakutanisha waandishi wa habari wa Radio za Kijamii kanda ya ziwa kwa lengo la kuwajengea uwezo namna ya kuielimisha jamii.

 Hata hivyo ukeketaji nchini Tanzania umetajwa kushamiri katika mikoa ya Manyara, Dodoma, Arusha, Mara na Singida hivyo jamii ya maeneo hayo inapaswa kuachana na ukeketaji ili kuwanusuru watoto wakike na madhara ya kiafya.

MWISHO