MADINI YA NICKEL KUWEZESHA AJIRA 3000.
March 24, 2021, 9:46 am
IMEFAHAMIKA kwamba uwekezaji wa madini ya Nickel wilayani Ngara sambamba na kujengwa kwa kinu cha kuchenjulia madini hayo ( Smalter )katika Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi,wilaya ya Kahama,mkoa wa Shinyanga,utawezesha kupatikana ajira za watu 3000.
Hayo yalibainishwa juzi wilayani Kahama,na timu ya Wataalamu wa Serikali na Muwekezaji wa Kampuni ya Tembo Nickel itakayochimba madini hayo,waliofika kuangalia na kubainisha eneo sahihi linalostahiki kujengwa Mtambo huo wa kuchenjua madini hayo yanayochimbwa wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Akiongea baada ya kubaini eneo sahihi,Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kabanga Nickel,Chris Showalter,alisema kukamiilka kwa ujenzi wa Kinu hicho,watu zaidi ya 1000,wanatarajiwa kuajiriwa katika Smalter hiyo itakayojengwa katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi katika halmashauri ya manispaa ya Kahama.
Aidha Showalter alisema uwekezaji huo kampuni ya Tembo Nickel,utanufaisha ajira takribani 2000 katika wilaya ya Ngara,mkoani Kagera mara shughuli za uchimbaji wa madini ya Nickel utakapoanza.