Madiwani watakiwa kupambania chakula shuleni
18 August 2023, 5:27 pm
Madiwani wamesisitizwa kuhakikisha upatikanaji wa chakula shuleni unazingatiwa.
Mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo amewataka madiwani kushirikiana na walimu kuhakikisha chakula kinapatikana shuleni ili wanafunzi wapate muda wa kutosha wa kujifunza.
Amesema hayo akiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani lililofanyika wilayani humo.
Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Igunga akiwemo diwani viti maalum Eva Godfrey na Diwani wa kata ya Bukoko Jidashema Mwandu wamesema watakwenda kusimamia suala hilo kwa kutoa elimu zaidi kwa wazazi na walezi juu ya umuhimu wa kuchangia chakula shuleni kwa ajili ya watoto wao.
Mkuu wa wilaya ya Igunga amesema Serikali ina lengo la kuhakikisha madarasa yote ya mitihani ya taifa wana pata chakula shuleni ili kuwapa nafasi nzuri zaidi wanafunzi kubaki shuleni kujifunza zaidi na hivyo kuongeza ufaulu kwenye masomo yao.