Uyui FM Radio

Uchunguzi miradi iliyokataliwa na Mwenge Tabora.

28 July 2021, 6:42 pm

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa TABORA imeanzisha uchunguzi kwenye miradi 3 kati ya 35 ambayo haikuzinduliwa wakati wa mbio maalumu za mwenge wa uhuru Mkoani hapa.

Akizungumza hii leo wakati wa kutoa Taarifa ya utendaji kazi kuanzia april hadi juni mwaka huu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa TABORA MUSA CHAULO amesema miradi hiyo inajumuisha hospitail ya wilaya ya TABORA.

Mkuu wa TAKUKURU TABORA Chaulo.
Sauti ya Chaulo.

Aidha Mkuu huyo wa TAKUKURU CHAULO amesema Taasisi hiyo itaendelea kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria kwa kushirikiana na wadau mbalimbali huku wakijikita katika utoaji wa elimu kwa wananchi.

Sauti ya Musa Chaulo.

Kwamujibu wa Taarifa ya TAKUKURU mkoani hapa uchunguzi katika miradi hiyo MITATU ambayo haikuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenye wa uhuru hivi karibuni utakamilika kwa kipindi cha julai hadi septemba mwaka huu.