Uyui FM Radio

Rc Tabora awa mbogo kusuasua ujenzi wa hospital ya Wilaya

26 April 2021, 5:45 pm

Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt Philemon Sengati ameiagiza Wilaya ya Kaliua  kukamilisha haraka mradi wa hospitali ya wilaya hiyo pamoja na ujenzi wa kituo  cha afya Usinge ili wananchi waanze kupata huduma za afya maeneo hayo.

Ametoa agizo hilo akiwa kwenye ziara ya kikazi wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya na kuagiza miradi hiyo inapaswa kukamilika kabla ya  juni 30 mwaka huu.

Dr.Philemon Sengati

Sauti ya Dr.Sengati

Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama amesema miradi hiyo imechelewa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya makisio ya vifaa kuwa chini tofauti na mahitaji.

mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama
Sauti ya Abel Busalama

Kwa mujibu wa viongozi hao kukamlika kwa hospitali ya wilaya pamoja na kituo cha afya cha usinge utakuwa na manufaa kwa wananchi kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya huduma za afya.