Uyui FM Radio

Wafanyabiashara Tabora wamlilia Hayati Dkt Magufuli

25 March 2021, 4:14 pm

Wafanyabiashara na wajasiriamali  katika Manispaa ya Tabora wamesema watamkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt John Pombe Magufuli kutokana na namna alivyo wapigania na kupata maeneo ya kufanyia biashara bila Bugudha.

mmjoja wa wafanyabiashara Sheila Chambuso

Wafanyabiashara hao akiwemo Haki Kasawa,Sheila Chambuso  na Muniru Butala wamesema Rais Magufuli mbali na kuwatetea wanyonge alihakikisha wafanya biashara pia wanajitegemea na kupata faida katika biashara zao ili kuendeleza Tanzania ya viwanda.

sauti za wafanyabiashara
  •  Naye  mratibu wa wajasiriamali   Mkoa  wa Tabora AShura Mwazembe   amesema  Hayati dkt John  Magufuli  alikuwa ni kiongozi wa  kipekee ambaye alikuwa akitamani maendeleo kwa wananchi  kwa ujumla.

Sauti ya mratibu wa wajasiriamali Tabora