Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 za Saccos ya Walimu kilosa zimepotea walio husika kuzitapika-Mrajis Shemdoe.
28 February 2021, 11:23 am
Chama cha ushirika Saccos ya Walimu Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kimepoteza fedha zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 baada ya wanachama na wanufaika wengine kukopa na kushindwa kurejesha kwa wakati kutoka mwaka 2007 hadi 2017 ambapo Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Morogoro Kenneth Shemdoe amemuagiza Mwenyekiti wa Saccos hiyo kuandaa orodha ya majina ya viongozi na watendaji wao ikiwemo namba za simu na mahali wanakopatikana ambapo walikuwepo kipindi hicho kwa kuzingatia muda aliokaa madarakani na kiasi cha fedha kilichopotea ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria .
Akizunguza katika kikao cha bodi ya Saccos ya Walimu Kilosa kilicho fanyika februari 26, 2021 katika ofisi ya chama hicho iliyopo katika jengo la ushirika Wilayani humo Mrajisi Shemdoe amesema kuwa inawezekana Viongozi hao na watendaji wake hawakuchukua hizo fedha lakini kwasababu walikuwa hawafuati taratibu, sheria na masharti ya chama basi watawajibika kwa mujibu wa sheria ya ushirika ,kifungu cha 126 na kwamba watalazimika kulipa faini kiasi cha shilingi Milioni 5 na kifungo kisicho pungua miaka miwili au vyote kwa pamoja ikiwa ni pamoja kuchanganya na upotevu au hasara aliosababisha katika chama .
Amesema kuwa fedha hizo ni za umma hivyo yeyote aliyeshiriki kuchukua hizo Fedha atazitapika na kwamba atahakikisha Fedha zitarudi kwa namna yeyote ile hakuna hata shilingi itakayo salia huko nje.
Aidha katka kikao hicho wajumbe wamekubaliana kwa pamoja kuweka mikakati kabambe ya kukiimarisha chama ambapo Shemdoe ametoa siku 30 kuanzia tarehe 1- 31 ndani wa mwezi machi mwaka huu kutekeleza maazimio hayo ambayo ni kuhakikisha chama kinaandaa orodha ya wastafu wote na kuanza kuwalipa kadri Fedha itakavyo patikana, kuongeza wanachama wapya, kutoa mikopo ya dharula ya muda mfupi ambayo itazalisha faida kwa haraka itakayo saidia kukiendesha chama ,kufanya taratibu za kupata leseni , kuandaa makisio au bajeti a kupitisha katika mkutano mkuu miezi miwili kabla ya mwaka wa fedha kuanza ,kuhakikisha hesabu za fedha
zinafika kwa mkaguzi wa nje ambaye ni mkaguzi wa vyama vya ushirika, Kutoa fomu za uchaguzi na kuhakikisha uchaguzi ufanafanyika kabla ya tarehe 31 April mwaka huu , kuwasilisha rasmi ya hesabu kila mwaka kabla ya tarehe 31 Januari , kuongeza hisa ,kufanya mikutano kwa mujibu wa sheria ikiwemo mkutano mkuu wa mwaka na kuhakikisha chama kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria za ushirika .
Hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa Saccos ya walimu Kilosa Issa Nyamkunga awali wakati akiwashilita taarifa take kwa mrajisi wa Mkoa amesema kuwa deni ni shilingi bilioni 1,685,554 ,178.59 ambalo limetokana na wanachama wenyewe ambao wametoka katika Makato yao kuanzia mwaka 2007-2017 ambapo wanadaiwa Kiasi cha shilingi milioni 157 na wengine hawakuingia katika makato kuanzia mwaka 2007-2017 pia wanadaiwa shilingi milioni 129, 608,873 pamoja na wanachama ambao mikopo yao ilichelewa kuiingia lakini wamemaliza madeni yao wananadaiwa shilingi milioni 480,028,352.62 na shilingi Milioni 910,515 ,926 ni deni la Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambako baadhi ya wanachama makato yao yanapitia huko hasa walimu .
Amesema kuwa katika deni hilo la zaidi ya shilingi bilioni 1.6 mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni 22 zimekusanywa na kuwekwa bank kupitia Mkusanya madeni (Tanfin) , ambaye ameingiza shilingi milioni 11, Takukuru Milioni 8.3 na milioni 3.3 zimelipwa kwa hiyali na wanachama wanao daiwa.
Hata hivyo Saccos ya walimu Kilosa ilisajiliwa mwaka 1999 kwa namba MG 240 kikiwa na jumla ya wanachama 190 na kiliendelea kuingiza wanachama hadi kufikia 1188 ambapo kwa sasa kina wanachama 247 .