Radio Jamii Kilosa
Radio Jamii Kilosa
30 September 2025, 3:18 pm

Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha taarifa wanazopokea au kuzitumia, zinakuwa sahihi na zimethibitishwa ili kuepuka kuchochea taharuki, chuki au migawanyiko isiyo ya lazima.
Na Asha Madohola
Katika kipindi maalumu kilichorushwa na Redio Jamii Kilosa, tulikuwa na Ndugu Daniel Samson, Mkuu wa Mafunzo na Utafiti kutoka Nukta Africa, alielezea kwa kina umuhimu wa kuthibitisha habari kabla ya kuzisambaza, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Ndugu Daniel alisisitiza kuwa katika kipindi cha uchaguzi, upotoshaji wa taarifa huongezeka kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidigitali, hivyo ni muhimu kutumia vyanzo vya uhakika, teknolojia za kuchunguza ukweli (fact-checking tools) na kuhoji chanzo cha kila taarifa kabla ya kuisambaza.
Aidha alitoa wito kwa wananchi na wanahabari kushiriki kikamilifu katika kampeni za kuelimisha umma kuhusu habari sahihi, ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya amani, ukweli na uwazi.