Kilele cha wiki ya wananchi Kilosa, Yanga wafanya usafi kliniki ya mama na mtoto
Kilele cha wiki ya wananchi Kilosa, Yanga wafanya usafi kliniki ya mama na mtoto
23 July 2023, 11:37 am
Kutoka kulia ni Makamo Mwenyekiti Tawi la Yanga Kilosa John Mwaluko na wa pili Katibu Mkuu Abdallah Pocho. Picha na Asha Madohola
Na Asha Madohola
Katika kusherekea kilele cha wiki ya wananchi Julai 22 wanachama na mashabiki wa Tawi la Yanga Kilosa Mjini wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira katika Kliniki ya Mama na Mtoto Kilosa.
Wananchi hao wa jangwani waliamua kuungana kwa pamoja ili kufanya shughuli ya kijamii yenye lengo na dhamira ya kuiombea mema na matokeo mazuri ya timu yao ya Yanga kwenye msimu mpya wa ligi kuu 2023/2024 ikiendeleza matokeo mazuri ya msimu uliopita kwa kutwaa mataji ya makombe yote yaliyowaniwa likiwemo kombe la ligi kuu Tanzania bara.
Katibu Mkuu wa Tawi la Yanga Kilosa Mjini Abdallah Pocho Sauti ya Katibu Mkuu wa Tawi la Yanga Kilosa Mjini Abdallah Pocho akizungumza Makamo Mwenyekiti Tawi la Yanga Kilosa Mjini Sauti ya Makamo Mwenyekiti Tawi la Yanga Kilosa Mjini John Mwaluko akizungumza Msaidizi Afisa wa Afya na Mazingira Hospitali ya wilaya ya Kilosa Mbaraka LilangaMsaidizi Afisa wa Afya na Mazingira Hospitali ya wilaya ya Kilosa Mbaraka Lilanga