Wakulima walalamika Kilosa
17 February 2023, 8:46 pm
Wakulima wilaya ya Kilosa wamelalamika kuchelewa kwa kupatiwa mbolea za ruzuku ile hali msimu wa kilimo umeshaanza na imefikia kipindi cha uwekaji wa mbolea katika mimea.
Na Asha Madohola
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mlimani Boma ililyopo kata ya Kasiki wilayani Kilosa Hosea Mgunda wakati akiongea na Redio Jamii Kilosa ambapo amesema imepita muda mrefu tangu wakulima wasijili katika ofisi ya Kata ila mpaka sasa hakuna kinachondelea.
Aidha ameiomba ofisi ya Kilimo kutoa maelekezo kwa wakulima suala la mbolea limefikia wapi kwani wananchi wamesubiri kwa kipindi kirefu bila ya kujua muafaka wa upatikanaji wa mbolea ya ruzuku umefikia wapi kwani hata kipindi cha kuweka mbolea kinakaribia kuisha.
Kwa upande wake Afisa Kilimo na Mratibu wa Mbolea Juma Mihenga amesema kuwa mpaka sasa wakulima 18,297 wameshajisajili kwenye mfumo na wamenufaika na changamoto iliyopo ni kuchelewa kwa wakulima kujiandikisha.
Mihenga amesema pia kuna changamoto ya mawakala na suala hilo ni la nchi nzima kwa kuwa wauza pembejeo wengi hawajajisajili katika mfumo hali inayopelekea kukosekana kwa mawakala wa kutosha.
Hata hivyo Mratibu huyo wa mbolea amewataka wakulima kutokupteza fursa ya kujiandiksha kwa kuwa serikali inampango wa kuikiinua kilimo na kumpunguzia gharama za mbolea mkulima kwani atapata kwa nusu ya bei iliyopo sokoni.