DC ataka heshima kazini, Narudi kufundisha Madrasa.
23 June 2021, 10:58 am
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Alhaji Majid Hemed Mwanga juni 22 2021 amewataka Viongozi wote Wilayani humo kuwa wabunifu pamoja na kufanya kazi kwa umoja, kushirikiana bila kubaguana wala kudharauliana kwani kwa kufanya hivyo Wilaya itasonga mbele zaidi kwa maendeleo.
Majid Hemed Mwanga ambaye ameteuliwa na Rais hivi karibuni kuwa Mkuu wa Wilaya Kilosa kuchukua nafasi ya Adam Mgoyi amesema Ili kuleta ufanisi katika kazi ni vyema kukawa na ushirikiano , kuheshimiana ,kwa watumishi wote kuanzia ngazi ya Mwenyekiti wa Kitongoji , Kijiji, Kata mbaka ngazi za juu.
Amesema kuwa hato mvumilia mkuu wa idara yeyote atakaye mdharau mtumishi na kusababisha manung’uniko kwa watumishi wa ngazi za chini anaye hitaji kupata huduma katika ofisi za Halmashauri na kuongeza kuwa haki ya mtu sio zawadi hivyo apewe haki yake anayo stahili kwa kujali utu na upendo kazini.
kwa upande wake mkuu wa Wilaya aliye maliza muda wake Ndugu Alhaji Adam Mgoyi amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kumteua Alhaji Hemed Majid Mwanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, huku akiwashukuru watumishi na wananchi wa Wilaya hiyo kwa ushirikiano waliompa kwa muda wote alipokuwa pamoja nao.
Amewataka watumishi na wananchi kwa ujumla kumpa Mkuu wa Wilaya mpya ushirikiano wa kutosha Ili waweze kusonga mbele katika kuwaletea wananchi maendeleo, pia amewaomba radhi watumishi kama Kuna mahali aliwakosea katika utawala wake kwani alikuwa katika kutekeleza majukumu yake kwakuwa alikuwa na dhamira njema ya kuijenga Kilosa mpya.
Mgoyi amesema kuwa kustaafu ni wajibu wa Kisheria na Kikatiba hivyo kila mtu atastaafu hivyo amemshukuri Mwenyezi Mungu kwa kumaliza kazi salama na sasa anarejea katika kazi yake ya awali kufundisha Madrasa kwani ni kazi ambayo imempa mafanikko makubwa hata kufikia hapo alipo, na bado aliendelea kuwa mwalimu kwa wengine.
Awali katika utamburusho uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa juni 22 mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Asajile Lucas Mwambambale ameeleza kuwa toka aingie katika Halimashauri ya Wilaya ya Kilosa inakaribia miaka mitatu sasa toka mwaka 2018 mwenzi wa 8 nilipo ingia katika Halmashauri imeweza kupiga hatua katika Maendeo kiuchumi na Elimu .
Amesema kuwa hali ya uchumi Kilosa imeongezeka kutoka bilion 2.2 na kufikia bilion 3.3 kwa mwaka wa fedha unaoishia 2020 ni ongezeko la bilioni 1.1 kwa kipindi cha miaka miwili ya utendaji wake na kuongeza kuwa kwa upande wa elimu Halmashauri imepanda kutoka nafasi ya mwisho Kimkoa katika Halmashauri 9 za mkoa wa Morogoro na sasa kuwa nafasi ya 5 kwa matokeo ya mwaka 2020 ambapo amesema kuwa amemkaribisha katika Halmashauri na yuko tayali kama Mkurugenzi wa Halmashauri kupokea maelezo na kufanya utekelezaji katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hatahivyo kikao hicho kilihudhuriwa na watumishi mbalimbali kutoka katika Halmashauri ya Wilaya Kilosa Wakuu wa Idara na Vitengo, taasisi za Kifedha ambapo Musa Haruni Meneja wa TRA Kilosa akizungumza kwa niaba ya taasisi nyingine amesema kuwa wako tayali kutoa ushirikiano kwa kwa Mkuu wa Wilaya Kilosa kwani hotuba yake imetoka Mwanga wa ushindi katika kupata mafanikko endapo wakishikamana kwa pamoja na kujituma kufanya kazi bila shuluti.