Huheso FM

Recent posts

September 27, 2021, 11:04 am

Mbunge wa Kahama mjini achangia ujenzi wa shule ya Sekondari Malunga

Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba amechangia millioni moja na laki moja kwa ajili ya kukunua matofali ya kukamilisha ujenzi wa sekondari ya Kata ya Malunga wilayani Kahama Mkoani Shinyanga iliyoanza kujengwa hivi karibuni. Akizungumza katika ziara yake…

September 22, 2021, 4:49 pm

Wananchi watakiwa kujitokeza ujenzi wa Bomba la Mafuta-Kahama

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga amewataka wananchi wilayani humo kuchangamkia fursa za mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta ambao unapita wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Akizungumza katika kikao cha wadau wa EWURA na TPDC ambacho kimeshirikisha wafanyabiashara na…

September 22, 2021, 3:18 pm

Jeshi la Zimamoto latumia gari moja kuhudumia halmashauri tatu

Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilayani Kahama mkoani Shinyanga limesema linakabiliwa na uhaba wa vifaa vya uokozi ikiwemo Magari. Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi hilo Hanafi Mkilindi wakati akizungumza na Huheso fm redio kuhusu mikakati ambayo wamekuwa wakiifanya katika…

September 20, 2021, 3:16 pm

Vikundi vyapewa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.

Wajumbe wa mradi wa mwanamke amka unaolenga kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto waliopo mashuleni Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia kwenye vikundi vyao. Hayo yamesemwa na…

July 26, 2021, 6:46 pm

Baiskeli 40 kusaidia kuzuia maambukizi mapya ya Ukimwi

Mabinti wenye umri kati ya miaka 15-24 wa halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga wamepatiwa Baiskeli zaidi ya 36 kwa ajili ya uelimishaji rika juu ya kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi. Baiskeli hizo zimetolewa na shirika la Huheso Foundation…

July 19, 2021, 8:00 pm

Machinga walionyang’anywa Matunda yao warejeshewa na Mkuu wa Wilaya

Kufuatia kukamatwa kwa wafanyabiashara wa matunda wa soko la Mkulima na kuonesha Migambo wakigombana na wauza matunda hao mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga ametatua Mgogoro huo. Akiongea na wafanyabiashara wadogo katika stendi ya CDT mkuu wa Wilaya, Festo…

July 19, 2021, 7:42 pm

DC Kiswaga: Maonesho ya kibiashara Kahama kuwa ya mfano

Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Festo kiswaga amewaomba wananchi wilayani humo kujitokeza katika maonesho ya Ujasiliamali na wafanybiashara wakubwa na wadogo katika viwanja vya halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani humo. Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake…

July 1, 2021, 9:54 am

Mwalimu wa tuisheni afungwa maisha jela Kahama

Mahakama ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga jana June 30, 2021 imemhukumu kifungo cha maisha jela, Baraka Andrea (25) mkazi wa Kata ya Mhongolo ambaye alikuwa mwalimu wa Tuisheni kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wake wa miaka nane. Akisoma hukumu…

May 31, 2021, 5:44 pm

Jambazi kutoka Dar es salaam auawa Shinyanga

Mtu mmoja anaejulikana kwa jina la Idd Masasi (43) anayedaiwa kuwa Jambazi ameuawa baada ya kupigwa risasi mguuni na mgongoni na askari polisi na alifariki wakati akipatiwa matibabu hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda…

May 27, 2021, 8:05 pm

Elimu ya hedhi salama kwa wasichana yazidi kutolewa wazazi waungana

Katika kuelekea siku ya hedhi salama duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi Mei 28 baadhi ya wazazi na walezi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameeleza namna wanavyotoa elimu juu ya makuzi kwa watoto wao wa kike. Wakizungumza na Huheso fm mapema…