FM Manyara
FM Manyara
5 February 2026, 1:36 pm

Na George Augustino
Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati, mbao pamoja na mabati yenye jumla ya thamani ya shilingi million 38 na laki tano kwa shule ya msingi kiongozi, shule ya msingi soraa, shule ya msingi singu B, pamoja na zahanati ya imbilili,zilizopo wilayani babati mkoani manyara.
Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya mkuu wa wilaya wa babati ambaye ndiye mgeni rasmi wa shughuli hiyo Emanuela Kaganda Meneja wa NMB kanda ya kaskazini Baraka Ladislaus amesema Benki ya nmb inatambua juhudi zinazofanywa na serikali na benki hiyo inaunga mkono juhudi hizo katika kuboresha huduma za maendeleo ya jamii ikiwemo elimu na afya kwa kutoa sehemu ya faida inayoipata.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Babati Emanuela Kaganda ameishukuru Benki ya NMB kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kuhudumia jamii kwa kutoa misaada mbalimbali pamoja na huduma za kifadha wanazozitoa kwa uaminifu kwa watumishi wa umma na jamii kwa ujumla.
Aidha Dc Kaganda Alisisitiza utunzaji wa vifaa hivyo hasa madawati hayo ili viendelee kuzisaidia shule hizo pamoja na kuahidi ushirikiano kati ya serikali na Bank ya NMB BABATI mkoani Manyara.
Naye Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiongozi mwalimu Omary Tindi ameishukuru Benki ya NMB kwa kuwasaidia madawati 50 ambayo yamesaidia kupunguza uhaba wa madawati katika shule hiyo na kuahidi kuendelea kuyatunza madawati hayo ili yaendelee kuwanafaisha wanafunzi wa shule hiyo.
