FM Manyara
FM Manyara
19 June 2025, 8:39 pm

Mtoto wa darasa la nne wa shule ya msingi Kiongozi kata ya Maisaka mkoani manyara, Prosper Gwai mwenye umri wa miaka 11, amefariki baada ya kugongwa na gari wakati akilekea shuleni.
Na Mzidalfa Zaid
Akiongea na fm Manyara mwenyekiti wa kitongoji cha Migungani Joseph Zakayo, amesema ajali hiyo imetokea leo june 19 majira ya saa kumi na mbili asubuhi ,katika kijiji cha Kiongozi, kata ya Maisaka wilayani Babati mkoani Manyara ambapo amesema mtoto huyo alikuwa akitokea katika kijiji cha Malangi kuelekea shule.
Nao baadhi ya majirani wa familia ya marehemu akiwemo ndugu na mwenyekiti wa kitongoji cha Malangi, wamesema tukio hilo limewasikitisha ambapo wameiomba serikali kuwajengea shule katika kitongoji hicho ili kuepuka changamoto zinazowakuta watoto kugongwa wakiwa wanaekea shuleni.
Aidha, FM Manyara inaendelea na jitihada za kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoani manyara Ahmed Makarani ili kuthibitisha tukio hilo.