Wanafunzi Kilosa waaswa kuacha kutumia mitandao ya kijamii
29 April 2023, 5:52 pm
Kutokana na matukio ya kujiingiza kwenye mapenzi ya jinsia moja wananchi wametakiwa kuwa makini na wageni ambao wanaowakaribisha majumbani mwao na kuwalaza katika vyumba vya watoto jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watoto kwa kufanyiwa vitendo visivyofaa.
“Wanafunzi hakikisheni mnakuwa mbali na mitandao ya kijamii kuangalia mambo yasiyofaa kwani ndio njia ambayo itakua rahisi kwenu kuepuka mimba za utotoni lakini pia kutojiingiza kwenye lindi la mapenzi ya jinsia moja yaani ushoga na usagaji”.
Na Asha Madohola
Jumuiya ya Wazazi wilayani Kilosa wamewataka wanafunzi kuacha tamaa na kufuatilia mitandao ya kijamii kwa kuwa ni vichocheo vitavyowaingiza katika matendo yaliyopo kinyume na maadili ya kitanzania na kuwapotezea malengo yao waliyojiwekea.
Hayo yamejiri katika ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilayani Kilosa Omary Ahmed Abdallah aliyefika katika shule ya Sekondari Mbumi iliyopo wilayani hapa na kupata fursa ya kuzungumza na wanafunzi hao ambao aliwaambia dunia imeangamia kwaa vitendo vya kikatili ikiwemo ubakaji naa ulawiti hivyo wanatakiwa waweze kujilinda na matukio hayo ambayo wakati mwingine yanafanywa na familia zao.
Akizungumza Katibu wa elimu na malezi afya na mazingira Kilosa Bi Lemna Hassan alisema kuwa lengo ya ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada za serikali kupinga wimbi la ushoga hivyo wameamua kuongea na wanafunzi na kuwapatia elimu ya kuepukana na matukio hayo ambayo watoto wengi wanaangamia kwa kubakwa na wengine ni tamaa za vitu vya anasa.
Bi Lemna alieleza kuwa katika kipindi hiki ambacho dunia imeangamia na ushoga wasikubali kulala na wageni ama ndugu zao kwa kuwa matukio hayo huanzia kwenye ngazi za familia, hivyo wanatakiwa kuzingatia masomo na kufuata maadili mema ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwa viongozi bora baadaye.
“Ushoga sio mzuri na ushoga hauendani na mila na desturi za kitanzania na hivyo mnatakiwa kutoa taarifa ukiona au ukifanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa sio vizuri na tunaunga mkono juhudi za serikali chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan kukemea ushoga” alisema Bi Lemna.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilayani Kilosa Omary Ahmed Abdallah alisema kuwa masuala ya ushoga yapo na dunia yote imekumbwa na janga la ushoga na nchi za Afrika zinalengwa kwa kuhamasishwa kuingia kwenye ushoga hivyo wanafunzi wanatakiwa kujihadhali kuingia katika mtego huo ambao utakua na madhara makubwa kwao.
Awali Katibu wa vijana chama cha Mapinduzi wilaya ya kilosa ndg Nyansio Gregory alisema kuwa kazi ya chama ni kuhakikisha watumishi na wananchi wanapatiwa haki za msingi bila kujali itikadi za kisiasa na aliwataka wanafunzi wawe wazi pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili ili serikali iweze kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika na kuacha kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ambavyo vipo kinyume na maadili ya kitanzania.