Wananchi wametakiwa kutunza na kuhifadhi mazingira
6 January 2021, 10:14 am
Akizungumza na Radio Jamii Kilosa Januari 6 ,2021 Afisa Mazingira Bwana Anthony Heriel Mbise amesema kuwa ni vyema wananchi wakatumia mvua zinazo endelea kunyesha kipindi hiki kupanda Miti na Maua.
Amesema kuwa Maua yanasaidia kupendezesha mazingira yanayo zunguuka na Miti inasaidia kuzuia madhara yatokanayo na upepo unao vuma kwa kasi, kupunguza hewa ya ukaa( carbodioxide ),kuzuia Mmomonyoko wa udongo na upatikanaji wa hewa Safi.
Mbise amesema kuwa kusafisha mifereji kutasaidia maji kutiririka Katika miundombi iliyo iliyo jengwa ili kuepuka maji kuingia kwenye makazi ya watu ambapo yanaweza kutuama na kusababisha mazalia ya Mbu.
Aidha maji hayo yanapopita juu ya mifyereji huharibu miundombinu ya barabara jambo litakalo pelekea serikali kuingia ghalama ya ukarabati wa barabara hizo.