Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan -Moropc.
7 April 2021, 10:45 am
Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro (MOROPC) kinampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuitaka Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kuvifungulia vyombo vyote vya Habari vilivyofungiwa na Serikali kwa Makosa mbalimbali.
Akitoa taarifa kwa umma Aprili 6 2021 Mwenyekiti wa Moropc Mkilanya Nikson baada ya kumalizika kwa Ghafra ya Rais Samia Hassani ya kuuwaapisha Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali na manaibu wake iliyo fanyika ikulu jijini Dar es salaam .
Mh Mw/kiti Mkilanya Amesema kuwa Mbali ya kutaka vyombo hivyo kufunguliwa Mh Rais Samia ameitaka Wizara hiyo kuimarisha Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini kwa ustawi wa utawala bora.
“Sisi kama chama kinachosimamia Taaluma ya Habari mkoa wa Morogoro tunaiona hatua hiyo ya Rais Samia Suluhu Hassan(SSH) kama ya kishujaa na kiukombozi kwa tasnia ya Habari na Wanahabari kwa ujumla ambayo wengi wao walionekana kukata tamaa katika utendaji na kuishi katika taaluma hiyo,”.
“Mbali na uamuzi na maelekezo hayo ni Imani kuimarika kwa tasnia yetu kutarejea na tunaamini ni hatua pia katika kuelekea kuinua ajira katika vyombo vya Habari ambazo kimsingi vingi vilishaanza kupotea kutokana na kufungiwa kwa vyombo hivyo,”.
Ameongeza kuwa zaidi ya yote tunamuomba Rais wetu mpendwa asaidie ushindani uliosawa katika matangazo ya biashara yanayotolewa kwa vyombo vya Habari vya Serikali na vile vya Binafsi ili vyombo vya binafsi vipate matangazo kutoka katika taasisi za Serikali na hivyo kuweza kujiendesha tofauti na hatua ya Sasa iliyopelekea vyombo vingi kufungwa kutokana na kukosa matangazo.
Aidha tunaamini Mh Rais akisimamia hayo Hali ya Ajira kwa wanahabari itaimarika kwa kuwa watakuwa na uhakika wa kipato.