Waadvendista wasabato wafanya matendo ya huruma -Kilosa.
20 March 2021, 4:05 pm
Waumini wa Kanisa la Waadvendista wasabato Kilosa lililoko Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wameadhimisha wiki ya huduma kwa jamii kwa kufanya matendo ya huruma kama vile kuchangia damu , kutoa mahitaji kwa watu wenye mahitaji maalumu , ikiwa ni pamoja na kufanya ibada ya pamoja kwa ajili ya kudumisha upendo .
Akizungumza machi 20, 2021 wakati wa kilele cha maadhimisho hayo Kiongozi wa vijana kanisa la Waadvendista wasabato Kilosa Salah Daudi Balula amesema kuwa wiki ya huduma kwa jamii ilianza toka tarehe 14 mach mwaka huu na kilele chake machi 20 2021 ambapo wameweza kuwafikia wahitaji wa aina mbalimbali ikiwemo wazee wasio jiweza katika kijiji cha Mkadage , Magomeni na Watoto wenye uhitaji katika Shule ya msingi mazinyungu .
Akifafanua zaidi Bi Balula amesema kuwa katika kuwaona wahitaji hao wameweza kutoa mahitaji kidogo kwa ajili ya kuwafariji kama vile Chakula ,Nguo ,mashuka ya kujifunika ,Viatu ,sabuni, chupa za chai za watoto,vifaa vya usafi ambapo vitu vyote vinathamani ya kiasi cha shilingi 400,000/= fedha iliyochangwa na vijana waumini wa kanisa la Waadvendista wasabato Kilosa na kuongeza kuwa wameweza kuchangia damu katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya wahitaji watakao fika Hospitali kwa ajili ya matibabu wakiwemo wanawake wajawazito.
Tito Mnkeni Kiongozi wa Vijana kanisa la Waadvendista wasabato kanda ya Kilosa ameongeza kuwa katika wiki hiyo ya maazimisho pia waliweza kutoa huduma kwa wazee wasio jiweza katika baadhi ya vijiji vya Kidete, Luhemba na Ulaya kulingana na uhitaji wa Mzee kama vile kufanya ukarabati wa Nyumba, kujenga choo na Kulima.
Nae Musa Haruni ambae nimiongoni mwa waumini wa kanisa hilo,ndie aliekuwa mkuu wa Msafara amesema kuwa vifaa vilivyo tolewa na ibada iliyofanywa kwa pamoja na wanafunzi wenye uhitaji katika shule hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kudumisha upendo wa dhati kati yao ambapo amewaomba wanafunzi hao wazidi kumuomba Mungu ili aweze kuwajalia mema kadri itakavyo wezekana katika maisha yao huku akiwapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayo ifanya ya kuwalea watoto hao na kuwataka kuendelea kufanya hivyo kadri watakavyo jaaliwa na Mwenyezi Mungu kwani hiyo ni ibada ya kweli katika utukufu wa Mungu .
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake wenye mahitaji maalumu Lakia Mkuyuyu amesema kuwa wanawashukuru Sana waumini vijana kutoka kanisa hilo kwenda kuwaona na kuwapelekea vitu ambavyo vimegusa sehemu ya mahitaji yao pia kufanya ibada ya pamoja kwao ni chakula charoho hivyo inawakumbusha kufanya maandalizi ya maisha mengine baada ya hapa Duniani na kwamba amewaomba waumini hao wasichoke kuwatembelea na kufanya ibada nao kila watakapo pata nafasi.
Awali Mwalimu Ally Mpulu Mkuu wa Kitengo cha wanafunzi wenye mahitaji katika shule hiyo amesema kuwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wako 87 ambapo 18 kati yao ni wenye uwalubino , 32 viziwi ,wasioona 28 uwoni hafifu 9 na kwamba wanatoka katika Mkoa wa Morogoro, Pwani na Dar es salaam.
Afisa ustawi wa jamii Kutoka Hospitali ya Wilaya Kilosa John Mpogole amesema kuwa katika tukio hilo la matendo ya huruma waumini wameweza kujitokeza kuchangia damu ambapo wamefanikiwa kupata dam chupa 16 ambazo zitasaidia kupunguza changamoto ya upungufuwa wa damu katika hospitali ya Wilaya na vituo vya afya kwani bado kunauhitaji mkubwa wa damu kulingana na mahitaji ya kila siku ambapo kwa mwezi hutumika chupa kati ya 60 Hadi 100 na inayonkusanywa kwa mwezi ni chupa 100-120 hivyo ameiyomba jamii kuendelea kuhamasika kuchangia damu salama kwa ajili ya kuokoa uhai wa watu wengine .