Bilion 1.27 kumaliza tatizo la maji kilosa-Injinia Chum.
16 March 2021, 11:44 am
Zaidi ya bilion 1.27 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maji safi na salama Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro ili wananchi waweze kupata huduma ya maji saa 24 kwa mwaka .
Hayo yamesemwa machi 16 2021 na Meneja wakala wa maji na usafi wa mazingira Ruwasa Wilayani kilosa Injinia Joshi Hamisi Chum alipokuwa katika kipindi cha mambo mseto kinachorushwa na Radio Jamii Kilosa wakati akizungumzia wiki ya maji ambayo huazimishwa kuanzi tarehe 16 machi hadi 22 machi kila mwaka.
Chum amesema kuwa Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1,270,000,000 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kumalizia miradi iliyopo katika vijiji mbalimbali wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mipya sehemu ambako bado kunachangamoto ya upatikanaji wa maji na kueleza kuwa kwasasa Ruwasa imefanikiwa kusamabazamaji kwa asilimia 73 kwa upande wa vijiji na mijini asilimia 85
Amesema kuwa ,kuna baadhi ya vijiji vinachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyanzo vya mazi kukauka, kutokana na shughuli za kibinadamu kama vile kilimo na uchimbaji wa madini ambapo tayali wameshaanza kufanya utafiti wa kubaini maeneo katika vijiji ambavyo havina maji safi na salama ili kuaza kuchimba visima virefu vitakavyo sambaza maji katika katika maene yapo .
Chum amefafanua kuwa maadhimisho wiki ya maji duniani kwa wilaya ya Kilosa itaadhimishwa kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzindua mradi wa maji Belega,kukagua uchafuzi wa vyanzo vya maji kata ya Ruaha,kukagua miradi ya maji inayo endelea maeneo ya , Kitete,Dumila,Mabwegere, kuhamashisha wananchi kutunza mazingira pamoja na kupokea changamoto za upatikanaji wa maji katika kijiji cha Tindiga .
Hata hivyo amesema kuwa kunabaadhi ya vyanzo vya maji vilivyokuwa vinasambaza maji katika mji wa Kilosa vimeharibika kutokana na mafuriko ya mto mkondoa ambavyo ni Nguzo sita na Mkondoa hali inayopelekea kuwa na changamoto ya kupatikana kwa maji katika baadhi ya maeneo na kusababisha mgawo wa mji na kuongeza kuwa jitihada zinafanika ili kubaini vyanzo vingine kumaliza tatizo hilo la mgao .