Radio Jamii Kilosa
Kilele cha wiki ya wananchi Kilosa, Yanga wafanya usafi kliniki ya mama na mtoto
23 July 2023, 11:37 am
Na Asha Madohola
Katika kusherekea kilele cha wiki ya wananchi Julai 22 wanachama na mashabiki wa Tawi la Yanga Kilosa Mjini wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira katika Kliniki ya Mama na Mtoto Kilosa.
Wananchi hao wa jangwani waliamua kuungana kwa pamoja ili kufanya shughuli ya kijamii yenye lengo na dhamira ya kuiombea mema na matokeo mazuri ya timu yao ya Yanga kwenye msimu mpya wa ligi kuu 2023/2024 ikiendeleza matokeo mazuri ya msimu uliopita kwa kutwaa mataji ya makombe yote yaliyowaniwa likiwemo kombe la ligi kuu Tanzania bara.