Huheso FM

Wananchi walalamikia ukosefu wa kizimba cha kuhifadhi taka

November 9, 2021, 8:48 pm

Wananchi wa Mtaa wa Sokola Kata ya Majengo iliyopo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wanakabiliwa na changamoto ya eneo maalumu la kuhifadhi taka hali inayopelekea kutupa taka hovyo katika eneo la mtu.

Wakizungumza na Huheso Fm wakazi wanaoishi karibu na eneo hilo wamesema wanapata changamoto wakati wa nvua kwani taka hizo zinatoa harufu kali na wapo hatarini kupata magonjwa ya milipuko.

Kwa upande wake Mkazi wa eneo hilo ambalo  wananchi wamegeuza kuwa sehemu ya kuhifadhi taka  Adonia Mhelo amesema mwanzo wazabuni walikuwa wanahifadhi taka na kuja kuzichukua baada ya mkataba wao kuisha na wananchi wakaligeuza eneo hilo kuwa dampo.

Amesema  watu wamekua wakitoka maeneo tofauti tofauti na kuleta      uchafu kwenye eneo hilo na taarifa alizifikisha katika serikali ya Mtaa huo na kusema watalifannyia kazi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Sokola amesema hajapata taarifa yoyote ya mtu anaelalamikian kutupa taka katika eneo lake hivyo ni wajibu wake wa kulinda eneo kutokana na sheria inavyoelekeza.

Hata hivyo baadhi ya maeneo ya mtaa wa sokola hakuna wazabuni wanao pita kwa ajili ya kuchukua taka kutokana na maeneo hayo kutopitikana kwa urahisi hali inayopelekea baadhi ya watu kutupa taka hovyo kwenye maeneo ya watu.