Huheso FM

Madarasa yatarajiwa kujengwa kwa mfumo wa force account.

October 30, 2021, 6:32 pm

Jumla ya madarasa 267 Wilayani Kahama mkoani Shinyanga yanatarajiwa kukamilika mwishoni  mwa mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga kuwa madarasa hayo yanatarajiwa kuanza kujengwa kwa kutumia mfumo wa force account kutokana na mfumo wa kutangaza tenda kuwa mrefu kulingana na uhitaji wa madarasa hayo.

Amesema fedha itakayotumika kukamilisha ujenzi huo ni fedha ambayo imetolewa na serikali kupitia mpango wa kukabiliana  na athari za  Uviko-19 ambapo wilaya ya kahama imepokea billioni  12.2 kati ya billioni 26.8 zilizopokelewa kwa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu huyo wa Wilaya, Festo Kiswaga amewataka watendaji na viongozi wengine wa serikali kusimamia ipasavyo fedha hizo ili kukidhi matakwa na itakapobainika mtumishi yeyote kukwamisha juhudi hizo za maendeleo hatasita kumkamata na kumuweka ndani.