Huheso FM

Mbunge wa Kahama mjini achangia ujenzi wa shule ya Sekondari Malunga

September 27, 2021, 11:04 am

Picha ya Mbunge jimbo la Kahma Mji Jumanne Kishimba

Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba amechangia millioni moja na laki moja kwa ajili ya kukunua matofali ya kukamilisha ujenzi wa sekondari ya Kata ya Malunga wilayani Kahama Mkoani Shinyanga iliyoanza kujengwa hivi karibuni.

Akizungumza katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa shule hiyo ya sekondari, Mhe. Kishimba amesema jitihada zilizopo ni kuhakikisha madarasa tisa yanayojengwa yanamalizika mapema ili kufikia January 2022 wanafunzi waanze kusoma katika shule hiyo.

Amesema kila sehemu anapita na kuchangia michango ya kukamilisha ujenzi wa shule pamoja na miundombinu mbalimbali ambapo katika shule ya msingi Malunga amechangia shilingi Laki mbili kwa ajili ya umeme na vyoo vya walimu ambavyo vimekua changamoto.

Sauti ya Mbunge jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Malunga, Emanuel Mloso amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kujitoa kuchangia ujenzi wa Maboma na wakikamilisha wataiomba halmashauri kumalizia ikiwa kwa hivi sasa milioni 66 zinahitajika ili kukamilisha maboma hayo.

Sauti ya mtendaji wa kata ya Malunga Emmanuel Mloso

Hata hivyo ujenzi wa shule hiyo ya sekondari umeanzishwa na wananchi wa Kata hiyo kwa kuchangia michango mbalimbali kwa ajili ya ujenzi huo.