Huheso FM

Uongozi wa Skauti Kahama waonywa kwa kushindwa kusimamia majukumu yake.

April 26, 2021, 5:19 pm

PICHA YA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA SKAUTI KAHAMA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama  mkoani Shinyanga, Annamringi Macha ameukosoa uongozi wa chama cha skauti ngazi ya Wilaya  ya Kahama kwa kushindwa kusimamia na kuendeleza skauti kwa baadhi ya shule.

Mkuu huyo wa Wilaya  ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Skauti Wilaya ya Kahama kwa walimu wa wakuu wa shule za misingi pamoja na maafisa elimu wilayani humo kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Kahama.

Macha amesema uongozi wa Skauti umeshindwa kusimamia kwani kuna baadhi ya shughuli ambazo zimekuwa zikiwakutanisha lakini wamekuwa hawaonekani hivyo amesema wahakikishe wanasimamia vyema kwani halmashauri zimekuwa zikitenga bajeti kwa ajili ya Skauti.

SAUTI YA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA

Kwa upande wake kamishna wa Skauti wilayani Kahama, Mussa Mohamed Chamma amesema kuwa katika halmashauri tatu za Wilaya ya Kahama za Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama ni halmashauri moja tu ndio imekuwa ikitenga bajeti hiyo ambayo ni Manispaa.

SAUTI YA KAMISHNA WA SKAUTI KAHAMA

Hata hivyo katika mafunzo hayo walimu wa kuu pamoja na maafisa Elimu wametakiwa kusimamia uanzishwaji wa vyama vya Skauti mashuleni ili kuweza kuwajengea uwezo watoto katika maadili ya ukakamavu.

MWISHO