Huheso FM

”Madiwani tungeni sheria ndogo ndogo za ujenzi holela” DC Kahama.

April 23, 2021, 10:36 am

Madiwani wa Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wameshauriwa kutunga sheria ndogo ndogo za ujenzi holela bila vibali kwa wananchi kupitia kwa mkurugenzi wa Manispaa hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Annamringi Macha wakati wa Baraza la Madiwanni la robo ya tatu ya mwaka huu.

Macha ameongeza kuwa viongozi wote wa serikali za mitaa washirikiane kwa pamoja  kubaini watu ambao wanajenga kiholela bila vibari ili wachukuliwe hatua.

Sauti ya mkuu wa Wilaya ya Kahama

Kwa upande wake Mrugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba amesema sheria ya kuwa na vibali vya ujenzi ipo lakini ambacho wanatakiwa kuboresha ni  kubandika vibali hivyo sehemu za wazi katika eneo la ujenzi hu

Sauti ya Mkurugenzi Manispaa ya Kahama

Baraza la madiwani halmashauri ya Manispaa ya Kahama limefanyika hii leo kupitia taarifa ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa pamoja na ambayo imekamilika.

Picha za madiwani wakiwa katika ukumbi wa Manispaa