FM Manyara

Kambi ya afya yazinduliwa Babati

26 March 2026, 22:36

Picha ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo (kulia) akitatazama mwanafunzi akipatiwa huduma ya afya

Kambi ya Afya ya matibabu ya siku sita imezinduliwa Rasmi leo kwenye Shule ya Msingi Oim Iliyopo katika kata ya Galapo Wilayani Babati mkoani Manyara iliyoandaliwa na Shirika la So They Can Tanzania.

Na Mwandishi Wetu

Akizungumza na Fm Manyara Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo amesema kambi hiyo itasaidia kuboresha afya za wananchi kwenye maeneo ambayo Yamekua yakifadhiliwa na Shirika la So They Can  Tanzania.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo

Kwa uoande wake, Meneja mkazi wa Shirika la STC  Roselyne Mariki amesema kambi hizo zimekuwa na mafanikio tangu kuanza  kwake hadi sasa na kwa mwaka huu wa 2026 wanatarajia kufanya kambi mbili za afya zitakazotoa huduma mbali mbali.

Sauti ya Meneja mkazi wa Shirika la STC  Roselyne Mariki

Kwa upande wake Mkuu wa msafara wa madaktari kutoka Hospital ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Sister  Thea Funto amebainisha kuwa wananchi wengi wanashindwa kufika kwenye Hospital kupata huduma za matibabu kwasababu yaukosefu wa Fedha.

Sauti ya Sister  Thea Funto

Kambi hiyo ya afya imekuwa na mafanikio mwaka hadi mwaka na mwaka huu huduma zinazotolewa ni pamoja na kupima na kupatiwa matibabu, ubainishaji wa watoto wenye Mahitaji maalumu, huduma za Upimaji wa macho, Huduma za ustawi wa Jamii na elimu ya Lishe na huduma za kinywa na Meno.

Picha ya wananchi wa kata ya gallapo wakipata huduma ya Afya