FM Manyara
FM Manyara
2 March 2026, 7:38 pm

Na Marino Kawishe
Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara imezindua maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo kiwilaya yatafanyika March 6 mwaka huu kwa kutembelea kituo cha kulea wazee kilichopo katika kijiji cha Saramee kata ya magugu na kupanda miti nakutoa baadhi ya Mahitaji ya kibinadamu kwenye kituo hicho.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Afisa maendeleo wa Halmashauri hiyo January Bikubwa amesema kauli mbiu ya mwaka huu inachochea ushirikiano wakutokomeza ukatili wa kijinsia na kulinda haki za kila mmoja hapa nchini.
Kwa upande wake msimamizi wa kituo hicho cha wazee na wasiojiweza Jackson Maige amesema hali ya kituo hicho ni nzuri na huduma zote muhimu ikiwemo matibabu kwa wazee zinazingatiwa na Tayari wamepata kadi za Bima ya afya kwa wote.
Naye Mkwenyekiti wa wazee kwenye kituo hicho Matias Yakobo ameshukuru Serikali kwakuwakumbuka na kuwapatia Mahitaji hayo.
Kiwilaya maadhimisho ya siku ya wanawake yatafanyika siku ya ijumaa March 6 kwenye kata ya Nkaiti na yatatanguliwa na kongamano la wanawake lenye lengo lakujadili masuala ya haki za wanawake na wasichana ambalo litafanyika March 3 mwaka huu katika shule ya msingi vilima vitatu kata ya Nkaiti Wilayani Babati.
