FM Manyara

Waadventisti wasabato Babati, watoa matibabu kwa wananchi wa Nakwa

26 February 2026, 2:13 pm

Picha ya Mratibu wa magonjwa yasiyoyakuambukiza kutoka hospital ya mji wa Babati Restituta Ngowi akizungumza na wananchi wa mtaa wa Nakwa

Zaidi ya Wananchi 116 kutoka kata ya Nakwa wilayani Babati mkoani Manyara wamefanyiwa  uchunguzi wa magonjwa mbali mbali ikiwemo kufanyiwa vipimo vya presha, kisukari na shinikizo la juu la damu zoezi ambalo limeendeshwa na kanisala la waadventisti wasabato mjini Babati.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kufanyiwa uchunguzi Mratibu wa magonjwa yasiyoyakuambukiza kutoka hospital ya mji wa Babati Restituta Ngowi amezitaja sababu zinazochangia kuongezeka kwa magonjwa yasiyo yakuambukiza kwa halmashauri ya mji Babati. 

sauti ya Mratibu wa magonjwa yasiyoyakuambukiza kutoka hospital ya mji wa Babati

Aidha Dokta Deogratius Panga ambaye amewafanyia vipimo wananchi hao amebainisha kuwa mtindo wa ulaji usio faa na kutofanya mazoezi ni viashiria vya magonjwa hayo huku akiitaka jamii kubadili mtindo huo.

Sauti ya dkt Deogratius Panga

Kwa upande wao wananchi wa Eneo hilo wamesema wamefurahishwa na huduma zilizotolewa kwa mda wa siku  tano. 

sauti za wnanchi wa nakwa