FM Manyara
FM Manyara
24 February 2026, 4:12 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameongoza kikao cha 40 cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Manyara ambacho kimehuduriwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi za serikali na Taasisi binafsi.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza katika kikao hicho Sendiga amesema mkoa wa Manyara umepokea zaidi ya shilingi bilion 700 kwa ajili ya kuboresha miradi mbalimbali ikiwemo maji, umeme, barabara n.k.
Amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa wa Manyara kuhakikisha wakulima wanapata taarifa sahihi za kilimo na mifugo ili kufahamu sehemu sahihi wanapata mbolea na mbegu za ruzuku.
Kwa upande wake katibu tawala msaidizi mipango na uratibu Lusungu Mwilongo amesema hali ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2025/2027 hadi kufika January 31 ni shilingi bilioni 25 sawa na asilimia 58 na ukusanyaji unaendelea ili kufikia lengo ifikapo mwezi wa saba mwaka huu.

Katika kikao hicho Taasisi mbalimbali zimewasilisha bajeti yao, ambapo kwa upande wa RUWASA, meneja wa RUWASA mkoa wa Manyara James Kionaumela amesema hadi kufikia December 25, 2025 upatikanaji wa maji ni asilimia 78.09.

Nae mkurugenzi wa BAWASA Idd Msuya, amesema mamlaka imetekeleza miradi mikubwa ya maji ikiwemo mradi wa DARAKUTA utakaosaidia wananchi wengi kupata huduma ya maji.

Aidha, meneja TANESCO mkoa wa Manyara Regina Mvungi , amesema katika mkoa wa Manyara jumla ya kata 142 zina umeme, vijiji 440, vitongji 1113 vimefikiwa umeme na vitongoji 833 havijafikiwa huduma ya umeme.
