FM Manyara
FM Manyara
19 February 2026, 1:55 pm

Mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wasio na uzalendo ambao wamekuwa wakiharibu miundombinu makusudi na kupelekea wananchi kukosa huduma.
Na Mzidalfa Zaid
Kaganda amesema hayo katika Baraza maalum la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Babati lililokutana kupitisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2026-2027, amesema kila mwananchi ana wajibu wa kulinda miundomninu ya serikali.
Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya madiwani kulalamikia changamoto ya kutokamilika kwa baadhi ya miradi, ikiwemo maji, umeme na afya ambapo wameiomba serikali kushughulikia changamoto hiyo.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya, ameitaka tarura kuhakikisha bara bara zote zinazotengenezwa zinawekwa mitaro ili kuepuka changamoto ya bara bara kuharibika mara kwa mara.

Aidha Naibu waziri, ofisi ya rais – menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, mhe. Regina Qwaray amewataka viongozi kutumia misingi ya haki, uwajibikaji na usawa.
