FM Manyara
FM Manyara
13 February 2026, 7:52 pm

Ayaren Lifestyle Hotel iliyopo mkoani Manyara imezinduliwa rasmi leo na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Taasisi , kampuni na maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara ambao wamejionea uwekezaji mkubwa uliofanyika mkoani hapa.
Na Mzidalfa Zaid
Akiongea katika uzinduzi huo Meneja wa hotel hiyo Allen Magese, amesema hotel hiyo ya kisasa itawahudumia wananchi kutoka maeneo mbali mbali ambapo amewaomba wanachi kufika hotelen hapo kujionea vivutio mbalimbali.
Katika ufunguzi huo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Mbulu Michael Semindu ambae amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Manyara, na kusema kuwa uwekezaji huo ni mkubwa katika mkoa wa Manyara, ambapo amempongeza mmiliki wa hotel hiyo kwa kuwa mbunifu.
Awali mwenyekiti wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) mkoa wa Manyara Mussa Msuya amesema hatua hiyo ya uwekezaji ni kubwa ambapo ameiomba serikali ya mkoa wa Manyara kutoa ushirikiano kwa wawekezaji kwa kuwawekea mazingira rafiki.