FM Manyara
FM Manyara
20 January 2026, 5:12 pm

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutumia mawakili na wanasheria wenye weledi katika utatuzi wa kesi mbalimbali ili changamoto zao zitatuliwe kwa wakati.
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa mkoa wa manyara Queen Sendiga, ameyasema hayo leo wakati akizindua kamati ya ushauri wa kisheria ngazi ya mkoa na wilaya na kliniki ya sheria bila malipo ambayo imefanyika wilayani hanang mkoani manyara na kuwataka wananchi kutumia klinik hiyo kuelezea changamoto zao za kisheria.
Kwa upande wake mkurugenzi wa uratibu na huduma za ushauri kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Neema Ringo, amesema kamati hizi imeanza kufanya kazi kuanzia january 19 hadi january 25 ambapo amesema zaidi ya wanasheria 30 wapo wilayani hanang kutoa huduma ya kisheria.

Mbunge wa jimbo la Hanang Asia Halamga amesema wilaya ya Hanang ni wilaya yenye changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi , hivyo kupitia klinik hii wananchi wengi watapata msaada wa kisheria.
Aidha, baadhi ya wananchi ambao wameudhuria klinik hiyo, wameishukuru serikali kwa kutoa msaada wa kisheria bure kwani klinik hiyo itasaidia kutatua changamoto zao.
