FM Manyara
FM Manyara
19 January 2026, 4:50 pm

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kamati ya ushauri wa kisheria ngazi ya mkoa na wilaya na kliniki ya Sheria bila malipo itakayofanyika wilayani hanang mkoani Manyara.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa na Leo na Mkurugenzi wa uratibu na huduma za ushauri kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Neema Ringo wakati akizungumza katika kipindi Cha mseto wa Leo kinachorushwa Fm Manyara redio.
Amesema kamati hizo zitakuwa za kudumu kwa Lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za kisheria , ambapo amewataka wananchi wenye changamoto ya kisheria kuzitumia kamati hizo kupatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wake mwanasheria wa serikali mfawidhi kutoka ofisi ya wakili mkuu wa serikali ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ushauri wa kisheria mkoa wa Manyara Lameck Butuntu amesema Lengo la kuunda kamati hizo ni kushughulikia kwa haraka malalamiko yanayotolewa na wananchi.

Nae mkuu wa kitengo cha Sheria ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara ambae ni katibu wa kamati ya ushauri wa kisheria mkoa wa Manyara Neema Gasabile amesema ofisi ya mkuu wa mkoa imekuwa ikipokea kesi nyingi , hivyo kupitia kamati hiyo malalamiko hayo yatatatuliwa kwa wakati.

Aidha , uzinduzi wa kamati hiyo utafanyika katika viwanja vya mount hanang wilayani hanang na mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga na huduma ya kisheria imeanza kutolewa Leo January 19 hadi January 25.
