FM Manyara

Khambay awashukuru wananchi kata kwa kata

7 January 2026, 4:30 pm

picha ya Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Mhe Emmanuel Khambay

Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Mhe Emmanuel Khambay ameanza ziara ya Kata kwa kata kuwashukuru wananchi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Na Marino Kawishe

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Singe Jan 6,2026 Mh Khambay amesema changamoto mbalimbali zilizopo kwenye kata hiyo ikiwemo ukosefu wa vivuko vya Barabara,ofisi, zahanati, umeme na maji zimeanza kutatuliwa  Ambapo amehaidi  kuchangia  tofali 1000 kwa ajili ya ujenzi ya ofisi ya Kijiji na tofali 1000 kwa ajili ya ujenzi ya nyumba ya daktari kwenye zahanati ya Singe.

Khambay amesema kwenye Jimbo lake ipo miradi mingi na ya kimkakati ambayo atahakikisha  inafanyiwa kazi na mamlaka husika ikiwemo mradi wa Barabara ya kutoka Kona ya Mrara kwenda mamire Hadi lango la Tarangire ambayo itaanza kwa lami kutoka Kona ya Mrara umbali wa mita 800.

Aidha amesema mradi wa kusafisha ziwa Babati kuna wataalamu kutoka Taasisi ya utafiti ya TPHRI wameshafika kufanya upembuzi na muda wowote kazi yakutoa magugu itaanza huku akiwataka Wananchi kutoa taarifa zenye uhakika ili anapofatilia kusitokee mgongano baina yake na Viongozi wengine.