FM Manyara
FM Manyara
15 December 2025, 4:15 pm

Katika msimu huu wa sikukuu, wafanyabiashara mkoani Manyara wametakiwa kuwa waaminifu kwa kutumia vipimo sahihi na kuacha kutumia vipimo batili ili muuzaji na mnunuzi wote wapate haki sawa.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yameelezwa leo na Meneja wakala wa vipimo mkoa wa Manyara Denis Misango wakati akiongea na fm Manyara, amesema katika kipindi cha sikukuu kumekuwepo na baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiharibu mizani makusudi kutokana na kuwepo kwa wingi wa watu wanaonunua bidhaa mbalimbali ambapo amewaonya wafanyabishara wa namna hiyo.
Aidha, amesema wanaendelea na kaguzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Manyara ili kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara watakaokaidi kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.