FM Manyara
FM Manyara
5 December 2025, 4:50 pm

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuitunza amani ya Tanzania na kuepukana na vurugu zinazosababishwa na baadhi ya watu wachahe ili kuijenga Tanzania yenye maendeleo.
Na Angel Munuo
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Manyara John Nzwalile wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM mkoa ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mkutano alioufanya na wazee december 02 jijini Dar es salaam.
Nzwalile amesema chama cha mapinduzi mkoa wa Manyara kimeunga mkono hotuba ya Rais Dr Samia aliyozungumza na wazee ambayo alisisitiza amani na mshikamano katika kuleta maendeleo kwa Taifa.
Aidha Nzwalile amewataka vijana kuilinda amani ya nchi iliyopo kwani ndio msingi wa maendelo kwa Tanzania na kutafuta njia nzuri ya kufikisha ujumbe na si kuandamana